Mmoja wa wapinzani
wakuu katika uchaguzi mkuu uliomalizika hivi punde nchini Uganda, Dkt
Kizza Besigye, amekatalia mbali matokeo ya uchaguzi huo, uliofanyika
siku ya Alhamisi.
Bw Besigye ambaye amekuwa akizuiliwa nyumbani
kwake tangu siku ya Ijumaa amesema kuwa raia nchini Uganda wameshuhudia
ulaghai mkubwa mno wa uchaguzi mkuu, kuwahi kufanyika katika taifa hilo
la mashariki mwa Afrika.Kanali huyo mstaafu ameelezea uchaguzi huo kama usio halali na kuwa ni mapinduzi ya kijeshi.
Rais wa muda mrefu Yoweri Kaguta Museveni, alitangazwa mshindi.
Rais Museveni ameiongoza Uganda kwa muhula wa tano mtawalia.
Wachunguzi wa kimataifa wanasema kuwa uchaguzi huo uliandaliwa katika mazingara ya hofu na kudhalalishwa.
Post a Comment