Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans Sports Club wameungana na watani wao wa jadi, Simba Sports Club kuyaaga mashindano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kukubali kichapo mbele ya Uganda Revenue Authority (URA) kwa njia ya matuta 4-3.
Mchezo huo wa nusu fainali ya pili ulifikia hatua ya matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1.
Yanga ambao walitawala mchezo huo kwa muda mrefu walipata goli lao mapema kabisa mwa mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake machachari Amiss Tambwe aliyefunga goli hilo kwa njia ya kichwa katika dakika ya 13 mchezo.
Kukosekana kwa umakini kwa wachezaji wa pande zote kulipelekea kupotezwa kwa nafasi nyingi za kupata magoli.
Kuelekea katika 15 za mwisho wa mchezo, URA waliongeza nguvu na hatimaye kupata Peter Lwasa alisawazishia timu yake katika ya 76.
Hatua ya matuta ilipofikia, Yanga walipoteza penati tatu huku URA wakipoteza penati moja tu na kufanya ushindi.
Wapigaji penati wa Yanga walikuwa ni Yondani, Msuva na Munishi ambao walufunga, huku Mwashiuya na Bussungu wakipoteza.
Wakati penati za URA zilipigwa na Kulaba, Kiyuyine, Otieno na Bwete ambao walifunga na Sikito akikosa tuta alilopiga.
Ushindi huo unawafanya URA kuingia katika hatua ya fainali na watachuana na timu ya Mtibwa Sugar iliyopata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Simba katika nusu fainali ya kwanza.
Post a Comment