Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa hababaishwi na hamu ya Pep Guardiola kuifunza kilabu hiyo.
Kocha huyo wa Bayern Munich ametangaza kwamba aitaihama kilabu hiyo mwezi Mei baada ya kuifunza kwa misimu mitatu.Mkufunzi huyo wa zamani wa Barcelona ameshirikishwa na kilabu zote mbili za Manchester pamoja na Chelsea na Arsenal.
Van Gaal mwenye umri wa miaka 64 yuko na kandarasi na kilabu hiyo hadi mwisho wa msimu ujao lakini kazi yake imekosolewa baada ya kucheza mechi nane bila ushindi katika ligi msururu ulioisha wikendi iliopita baada ya kuishinda Swansea 2-1.
Post a Comment