Dk Shein akishuka katika gari la kijeshi alilotumia kuwasalimia wananchi |
Mamia ya wananchi wa mikoa mitano ya Unguja wamejitokeza kwa wingi kusherehekea
miaka 52 ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kufurika kwa wingi katika uwanja wa Amaan
mjini hapa.
Maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya Unguja waliopita mbele ya mgeni rasmin
rais wa Zanzibar dk.Ali Mohamed Shein na wageni mashuhuri,ngoma ya asili za
utamaduni wa watu wa Unguja na gwaride rasmin la vikosi vya ulinzi vikiongozwa na
jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ,ni baadhi ya matukio yaliyowavutia wananchi wengi
waliofika katika kiwanja cha Amaan.
Wananchi walianza kuingia katika uwanja wa Amaan kuanzia majira ya saa moja ambapo
milango ilianza kufunguliwa na kuruhusu wananchi ikiwemo waliotoka katika kisiwa cha
Pemba hadi kufika saa 4 ulionekana wazi wazi kuzidwa na idadi kubwa ya wananchi
ambao walibaki nje ya uwanja.
Meli mpya ya MV.Mapinduzi ilifunga safari kwenda katika kisiwa cha Pemba kwa ajili
ya kuchukuwa wananchi ili kupata nafasi ya kuhudhuria sherehe hizo
'Yadumu mapinduzi ya Januari 1964 ni maneno yaliyoandikwa katika baadhi ya mabango
yaliyobebwa na waandamanaji waliopita mbele ya mgeni rasmin wakimaanisha kwamba
watayalinda mapinduzi kwa nguvu zote.
Viongozi maarufu wa kitaifa walianza kuingia katika majira ya saa 2.30 ambapo
viongozi waliotia fora na kushangiliwa kwa nguvu zote ni rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania John Magufuli ambaye mara tu alipoingia alipigiwa wimbo wa taifa.
'Hapa kazi tu'ni sehemu ya kauli zilizosikika kutoka kwa wananchi ambao
walimkaribisha rais Magufuli ambaye hiyo ilikuwa mara yake ya wanza kuhudhuria
sherehe za Mapinduzi akiwa rais wa Muungano.
Baadhi ya wananchi waliohojiwa walikiri na kusema sherehe za miaka 52 zimefana licha
ya wafuasi wa chama cha CUF wakiongozwa na makamo wa kwanza wa rais maalim Seif
Sharif Hamad kususia.
Maalim Seif Pamoja na mawaziri wanaounda serikali ya umoja wa kitaifa kutoka CUF
wamesusia sherehe hizo kwa kile kinachoelezwa kutoridhishwa na maamuzi ya tume ya
uchaguzi ya zanzibar ZEC kufuta uchaguzi wa Oktoba 25.
Vijana wa Chama cha
Mapinduzi wakibeba Picha la Marehemu Rais wa
Kwanza wa Zanzibar Mzee
Abeid Karume wakati wa Maandamano ya kusherehehekea
Kilele
cha Mapinduzi Kutimia miaka 52 leo |
Post a Comment