Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es salaam amewatahadharisha wananchi kutobeba kiasi kikubwa
cha fedha kutoka benki bila kuwa na ulinzi.
Ameyasema hayo leo
jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
operesheni kali inayoendelea ya kukabiliana na wimbi la uhalifu.
Kamishna Simon Sirro
amewasisitiza wananchi kuacha tabia ya kuchukua kiasi kikubwa cha fedha kwakua
wanatahadharisha maisha yao.
“kuna namna nyingi za
kuhamisha fedha zikiwemo za kutumia mitandao ya simu,ni vizuri kutumia njia
hizo kuliko kubeba fedha mkononi bila ulinzi”alisema Sirro.
Aidha, Kamishna Sirro
amewataka wananchi wanaochukua fedha kwa kiasi kikubwa kutoka benki
wasindikizwe na polisi ili kulinda usalama wao na mali zao
.
Pia ametoa rai kwa
wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za waalifu
ili kuondoa wimbi la uhalifu linaloendelea kushamiri siku hadi siku.
Jeshi la Polisi kanda
maalum ya Dar es salaam linaendesha oparesheni katika mikoa yote ya kipolisi
iliyoanza mwishoni mwa mwezi Desemba ambayo inahusisha ukamataji wa majambazi,
waporaji wa kutumia pikipiki na wahalifu wengine.
Source: Jacquiline
Mrisho MAELEZO
Post a Comment