0

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara Fortunatus Mathew Kagoro akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.


Na Clarence Chilumba,Masasi.
MKURUGENZI wa Halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara Fortunatus Kagoro amewaondoa hofu madiwani wa halmashauri hiyo kuhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika kuwahudimia wananchi.
Kagoro ameyasema hayo jana wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa karakana ya maji mjini hapa.
Alisema atahakikisha kuwa anashirikiana bega kwa bega na madiwani wa halmashauri katika kufanya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ili kuweza kuwahudumia wananchi hatimaye kuifanya Masasi kuwa nuru ya  maendeleo wilayani humo.
Kagoro alisema anaamini watendaji wake katika halmashauri hiyo hawatafanya kazi kwa kuangalia itikadi za vyama bali watakuwa na ushirikiano mzuri na madiwani hao kutimiza malengo ya halmashauri.
Aliongeza kuwa atahakikisha suala la mapato linakusanywa vema na halmashauri kwa kushirikiana na madiwani hao pamoja na watendaji wake ili kuweza kuwa na  mapato ya kutosha yatakayoifanya iweze kutoa huduma kwa wananchi.
Ondoeni hofu madiwani mimi nitafanya kazi na nyinyi kwa kushirikiana pamoja ili halmashauri yetu tupate maendeleo kwa kasi nakushukurui sana tangu tumeanza tunashirikiana vizuri,”alisema Kagoro.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Sospeter Nachunga alisema ushirikiano ni jambo jema kati ya madiwani na watendaji na kwamba hatua hiyo itasaidia kuifanya halmashauri kuwa na maendeleo.
Alisema madiwani wanapaswa kuweka kando itikadi za vyama vyao badala yake wafanye kazi kwa kuangalia maslahi ya Masasi.

“Nashukuru tangu nianze kuongoza halmashauri hii sijaona mpasuko baina ya madiwani na hata kwa upande watendaji tunafanya kazi vizuri na kushirikiana na nawapongeza sana kwa hili,”alisema Nachunga
Alisema bila kuwa na ushirikiano kati ya watendaji wa ofisi ya mkurugenzi na madiwani itakuwa vigumu kupata maendeleo ambayo kila mara wamekuwa wakikaa vikao kwa ajili ya kujadili hivyo nguvu ya pamoja ndio nyenzo ya maendeleo.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top