Meya
wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob
akiwasili katika jengo la ofisi yake tayari kwa kuanza kazi rasmi.
Pichani akisalimiana na maafisa wa Manispaa hiyo ya ardhi. (Picha zote
na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Modewjiblog team
Meya
mpya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob,
ameanza majukumu yake mapema leo 18 Januari ya Umeya huku akikumbana na
umati wa wananchi waliofika kumuona kwa malalamiko ya migogoro ya ardhi
ambayo ni changamoto katika Manispaa hiyo.
Hata
hivyo Meya huyo baada ya kuwasili ofisini kwake na kupokelewa na baadhi
ya maafisa kadhaa wa Manispaa hiyo na kutinga kwa mara ya kwanza ndani
ya ofisi ya Meya ambayo atakuwa akiitumia kwa kipindi chote, baada ya
saa chache kundi la wananchi kutoka Wazo Block B, walifika katika ofisi
hiyo kwa lengo la kumuona ilikumweleza kero zao ambazo wamedai kuwa
wafanyakazi na watendaji wa Manispaa hiyo wamepora maeneo yao na
kuwauzia wafanyabiashara wengine.
Kwa
busara ya Meya Boniface Jacob, ameweza kusikilza kero za wananchi hao
huku akiahidi kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu hadi hapo haki
itakapopatikana. Ambapo amewaomba wananachi hao wasubirie kuona kama
Manispaa ilifanya tathimini na nani aliuza viwanja hivyo na fedha
ziliingia wapi ambapo ametoa agizo kwa Mtathimini na afisa ardhi wa
Manispaa kuanza mara moja kukagua kujua nani ameusika kwenye mgogoro.
Wakazi
hao zaidi ya 50, wanaeleza kuwa, mgogoro huo umeendelea kudumu zaidi ya
miaka 15 sasa huku mara zote wamekuwa wakizungushwa pasipo kupata haki
zao. Pia wameeleza kuwa, miongoni mwa wananchi wanaokaa kwenye maeneo
hayo wamekuwa wakiishi kwa hofu ya kuvunjiwa nyumba zao kwani baadhi ya
watu wamekuwa wakifika na kuwapa taarifa kuwa maeneo hayo ni ya
mwekezaji huku wengine wakitumia ubavu kuvunja nyumba za wananchi
pasipokuonyesha hati halisi kitendo ambacho wamekiona kuwa Watendaji wa
Manispaa hiyo kuuza kinyemela viwanja vyao.
Pia
wananchi hao wamewataia baadhi ya vigogo wa Serikali wakiwemo watendaji
wa Manispaa hiyo ya Kinondoni kwa kujimilikisha maeneo ikiwemo kujenga
nyumba katika ardhi ya wananchi hao.
“Karibu Mh. Meya.”
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob akiwa
katika mazungumzo na wananchi hao wa Wazo Block B ambao walifika katika
ofisi ya Meya huyo kumueleza mgogoro wao wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya
miaka 15 sasa dhidi ya Manispaa ya Kinondoni inayolalamikiwa kuuza
kinyemela maeneo yao na kuwapa watu wengine.
Baadhi
ya wananchi wa Wazo Block B ambao walifika katika ofisi ya Meya huyo
(hayupo pichani) kumueleza mgogoro wao wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya
miaka 15 sasa dhidi ya Manispaa ya Kinondoni.
Post a Comment