Uongozi wa Mkoa wa Singida umefuta matumizi ya zaidi ya Sh60 milioni kwa
ajili ya kugharamia sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya mkoa huo
tangu kuanzishwe kwake.
Sherehe hizo zilitarajiwa kufanyika Oktoba 15 baada ya wadau mbalimbali kuombwa kuchangia fedha hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone alitoa taarifa hiyo juzi, wakati akiwatakia wananchi heri ya Krismasi na Mwaka Mpya kupitia vyombo vya habari.
Alisema badala yake fedha hizo zitatumika kununua vifaa tiba na vitendea kazi katika hospitali mpya ya rufaa.
“Baada ya Uhuru, Mkoa wa Singida ulikuwa umeunganishwa na Dodoma na kupewa jina la Central Province, lakini sasa unajitegemea na uligawanywa mwaka 1963.
“Kwa bahati mbaya maadhimisho hayakufanyika kutokana na sababu mbalimbali, tuliyemtarajia kuwa mgeni rasmi kwa wakati huo, Rais mstaafu Jakaya Kikwete alikuwa na majukumu mengi ya kitaifa na kimataifa,” alisema Dk Kone.
Alisema baada ya ofisi yake kubaini kuwa sherehe hiyo imepitwa na wakati, waliwaita wadau wote waliochangia na kukubaliana fedha hizo zitumike katika shughuli nyingine ya maendeleo.
Hata hivyo, baadhi ya watu walidai kuwa uamuzi huo ni ishara ya kuunga mkono agizo la Rais John Magufuli ya kuachana matumizi yasiyo ya lazima, badala yake fedha husika zitumike kwa maendeleo ya wananchi.
Mbali na Dk Kone, wengine waliowahi kuwa wakuu wa mkoa huo ni Dantes Ngua, Peter Kisumo, Rajabu Semvua, Kapilima Kapilima, Kingunge Ngombale- Mwiru na Moses Nnauye.
Wengine ni Charles Kilewo, Brigedia Silas Mayunga, Abdallah Nungu, Kapteni Peter Kafanabo, Profesa John Machunda, Meja Jenerali Mwita Marwa, Gallus Abeid, Abubakar Mgumia, Kanali Anatoly Tarimo na Halima Kasungu.

Post a Comment