Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibaz akimkabidhi mshindi ambaye ni Mwalimu
wa Shule ya St. Jude Mkoani Arusha aliyeambatana na familia yake,
Rasul Mngazija gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya Sh. Milioni 12
katika promosheni ya jishindie IST iliyofanyika jana jijini Arusha
iliyoendeshwa na kampuni ya uuzaji magari ya Be Forward Tawi la Tanzania
Muonekano wa Gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya Sh. Milioni 12
Mshindi
Rasul Mngazija akiwa na mkewe Hazina Msechu wakiwa na nyuso za furaha
ndani ya gari aina ya IST walioshinda katika promosheni iliyokuwa
ikiendeshwa na kampuni ya Be Forward Tanzania
Rasul Mngazi akiwa ndani ya gari akijaribu kuwasha huku akiwa na uso wa tabasamu
Afisa
masoko kampuni ya Be Forward tawi la Arusha Gooluck Lyimo akiwa
anamkabidhi mshindi documenti za gari ofisini kwao jijini Arusha jana
mara baada ya kutembelea ofisi hizo
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibaz akionyesha documenti za
gari kwa waandishi wa habari pamoja na wadau waliofika jana katika
promosheni hiyo ya Shinda Gari
Afisa Masoko Shufaa Kilango akiwa anatoa maelezo kwa ugeni uliotembelea ofisi zao jana jijini Arusha
Muonekano wa ndani wa ofisi za Be Forward jijini Arusha
Aliyeshika
mfuko ni mkurugenzi wa jamiiblog Pamela Mollel akiwa na timu nzima ya
Be Foward Arusha pamoja na mshindi wa gari IST akisindikizwa na familia
yake
Familia ya Be Forward wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi
Wafanyakazi wa Be Forward wakiwa katika nyuso za furahaaaa
Rasul
Mngazija akiongea katika halfa hiyo ambapo alisema kuwa “Sikutegemea
kwanza kama ntakuwa mshindi kwani nilifika katika ofisi zao kwa ajili ya
kuagiza gari nyingine,”
Meneja Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibaz akiongea katika ofisi za Be Foward jijini Arusha
Mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi na Citizen Musa Juma akiangalia zawadi alizopewa na kamapuni hyo
Mshereheshaji
wa halfa hiyo Akida ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha Radio 5
akifanya yake katika ofisi za Be Forward jijini Arusha(Picha na Pamela
Mollel wa Jamiiblog Arusha)
Mwalimu
wa Shule ya St. Jude iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha Rasul
Mngazija ameshinda gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya Sh. Milioni
12 katika promosheni iliyofanyika jijini Arusha iliyoendeshwa na kampuni
ya uuzaji magari ya Be Forward Tawi la Tanzania
Akizungumza
Mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo jana katika ofisi za kampuni hiyo
Mwl. Mngazija aliyekuwa ameongozana na famlia yake kupokea zawadi hiyo
aliishukuru BE Forward kwa kumchagua kuwa mshndi katika promosheni
hiyo.
“Sikutegemea kwanza kama ntakuwa mshindi kwani nilifika katika ofisi zao kwa ajili ya kuagiza gari nyingine,”
“Nikiwa
hapo ndipo waliponijulisha pia kwamba kuna promosheni wanaendelea nayo
kwa wateja wanaoagiza magari kupitia kwenye ofisi zao. Kwa hiyo nilijaza
fomu na kuendelea kusubiria,”
Mngazija
aliendelea kusema kwamba kufanikiwa kuibuka mshindi wa zawadi hiyo gari
kumemuongezea chachu ya kuhamasisha watu wengine zaidi kutumia huduma
za kampuni hiyo kwa kuwa balozi wa Be Forward
Kwa
upande wake Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey
Mibazalisema kwamba kampuni hiyo itaendelea kuwa karibu zaidi na jamii
katika shughuli zake ikiwamo kurudisha sehemu ya faida inayopatikana.
Alisma
baada ya kufungua ofisi zao jijini Dar es Salaam sasa wamefungua katika
jiji la Arusha lengo likiwa ni kuwasogezea huduma zaidi wananchi.
Katika
uzinduzi huo ulioambatana na kumkabidhi gari mshindi, Geofrey aliwataka
watanzania na watu wengine wanaopanga kununua magari kutumia zaidi
kampuni hiyo kwa ajili ya usalama wa fedha na mali zao.
“Mtu
yeyyote anayekuja kuagiza gari ofisini kwetu tunampa ushauri wa bure,
wa aina gani ya gari anatakiwa kuagiza masuala ya kodi,”
Pia
aliongeza kuwa wanatoa huduma ya ushauri kwa wateja wao kabla ya kuagiza
gari huku akiwataka wananchi kutumia kampuni hiyo kuagiza magari
kwakuwa usalama upo wa kutosha ukilinganisha na wajanja wa mjini
Post a Comment