0




Jumapili ni siku muhimu ya kuhitimisha harakati za kisiasa zilizodumu kwa takribani miezi sita ikijumuisha kutangaza nia, kuchukua fomu, kutafuta wadhamini, uteuzi ndani ya vyama mpaka kampeni za majukwaani. Kufanikisha hilo, unatakiwa kufahamu yafuatayo:
Kura iliyoharibika ni ile ambayo;
1. Haina alama yoyote.

2. Imepigwa kwa wagombea zaidi ya mmoja,

3. Imeandikwa jina la mpiga kura,

4. Alama imewekwa nje ya kisanduku cha picha

ya mgombea

5. Haina muhuri wenye alama rasmi

Kura sahihi;

1. Yenye alama ya ‘v’ kwenye kisanduku.

2. Yenye alama yoyote kwenye kisanduku/picha/ jina la mgombea.
Kutakuwa na utata endapo utaweka alama iliyopitiliza kisanduku cha mgombea mmoja na kufika kwa
mwingine. Epuka kuharibu kura. Kura yako, mustakabali wako

Post a Comment

 
Top