0
 
Raia washerehekea taifa lao kutangazwa kwamba halina ebola
Maelfu ya watu wa Sierra Leone wameteremka katika barabara za mji mkuu, Freetown, kusherehekea kuwa zimepita siku 42 bila ya mtu yeyote kuuguwa ugonjwa wa Ebola.
Wengi walikusanyika kwenye mti mkubwa wa pamba, baadhi yao waliwasha mishumaa kukumbuka wale waliokufa; na wengine walicheza kwa furaha.
Shirika la Afya Duniani limethibitisha rasmi, kuwa nchi hiyo sasa imetokomeza Ebola.
Ebola iliuwa watu zaidi ya elfu nne Sierra Leone, katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu.
Maelfu ya watoto wameachwa yatima, na uchumi umeporomoka.
Rais Ernest Bai Koroma amesema huu ni mwisho wa safari ngumu.

Post a Comment

 
Top