Mshambuliaji akamatwa Colorado
Watu 3 wameuawa
baada ya kupigwa risasi na mtu mmoja aliyevamia kituo cha kupanga uzazi
katika eneo la Colorado Springs nchini Marekani.
Kituo hicho kinasimamiwa na shirika la kitaifa la afya la Planned Parenthood ambalo limekuwa likilaumiwa na baadhi ya watu kwa kutoa mimba.
Risasi za kwanza zilisikika mapema asubuhi na kuendelea kwa saa tano polisi wakifyatuliana risasi na mtu huyo.
Polisi walifyatuliana risasi na mtu huyo walipokuwa wakiwaokoa watu waliokuwa wamekwama katika jengo hilo.
Wengine wao walikuwa na majeraha.
Afisa wa polisi wa kutoa usalama katika Chuo Kikuu, Garrett Swasey, mwenye umri wa miaka 44, alikuwa miongoni mwa waliouawa asubuhi.
Alikuwa na mke na watoto wawili.
Watu wengine tisa, kukiwemo maafisa wengine watano wa polisi walipelekwa hospitalini na inasemekana kuwa hali yao inaendelea kuimarika.
Baadaye mwanamume mmoja alijisalimisha na kutiwa mbaroni na kuelekezwa kwenye kituo cha polisi.
Hata hivyo kufikia sasa lengo hasa la shambulio hilo halijulikani.
Post a Comment