Mganga Mkuu wa
Wilaya ya Liwale amewatadharisha wananchi wote kuchukua tahadhali dhidi ya
ugonjwa wa kipindupindu ambao unaambukiza kwa kunywa maji au chakula chenye
vimelea vya kipindupindu.
Ugonjwa huu unaua ndani ya saa sita (6) TANGU
MGONJWA APATE MAAMBUKIZI.
TAHADHALI
HII INALETWA KWENU KUTOKANA NA UGONJWA HUU KUTOKEA WILAYA YA KILWA MKOANI LINDI.
DALILI ZA
KIPINDUPINDU
>Kuharisha na kutapika mfululizo,kinyesi cha mgonjwa wa
kipindupindu kinakuwa chepesi cha majimaji yanayofanana na maji yakuoshea
mchele ambapo kinapelekea kupoteza nguvu kwa mgonjwa kutokana na kupoteza maji
mwilini.
JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU
>Kunywa maji yaliyochemshwa
>Kula chakula cha moto
>Nawa mikono kwa maji safi na sabuni baada ya
kutoka chooni
>Nawa mikono kabla ya kula
>Kutopeana mikono wakati wa kusalimiana
>Kuto mwaga maji machafu hovyo
>Kutojisaidia hovyo mtoni na katika vyanzo vingine
vya maji
>Kutonyweshea mifugo mtoni
>Kutolisha mifugo kandokando ya mto
>Kutofua nguo karibu na vyanzo vya maji/mtoni
>Kutoosha magari na pikipiki kandokando ya mto
>kuto kula matunda hovyo barabarani kwani maji
yanayotumika kuosha matunda sio safi na salama
USHAURI
>Mtu yeyote mwenye dalili za ugonjwa huu afikishwe
haraka kituo cha kutolea huduma za Afya kilichopo karibu na pia mgonjwa
anatakiwa apewe maji ya kunywa kwa wingi wakati taratibu za kumfikisha mgonjwa
kituo cha afya zinaendelea.
Tangazo hili limetolewa na
Dr.Martin Mwandiki
Kny;Mkurugenzi Mtendaji(W)
LIWALE
Post a Comment