Polisi
katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu wameripotiwa kuua watu saba wakati
wa shuguli ya mgao wa chakula cha msaada katika kambi moja ya wakimbizi.
Shahidi mmoja amesema wanawake ni kati ya waliouawa.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko amesema maafisa wa polisi walianza kugombana kabla ya kuanza kufyatuliana risasi.
Watu
wengine 12 walijeruhiwa katika makabiliano hayo baina ya maafisa hasimu
walipokuwa wakisubiri kugawanyia kadi na vibali vya kuwaruhusu kupokea
vyakula vya msaada.
''kulitokea
ufyatulianaji wa risasi kati ya maafisa wa polisi waliokuwa wakilinda
bohari la vyakula vya msaada na maafisa wa jeshi''alisema Mohamed Burhan
ambaye ni afisa wa Polisi.
''raia 7 waliuawa katika makabiliano hayo nje ya Mogadishu''
Waliouawa ni pamoja na watoto na wanawake na wanaume wazee.
Image copyrightImage caption7 wauawa wakisubiri chakula cha msaada Somalia
Mwakilishi
wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nick Kay alielezea kughadhabishwa na
mno na mauaji hayo ya watu waliokuwa na njaa wakitafuta chakula cha
msaada''
''Sharti haki ifanyike dhidi ya wale waliotekeleza mauaji hayo''
Mauaji hayo yalitokea mjini Afgoye nje ya mji mkuu wa Mogadishu.
Hadi kufikia sasa haijulikani ni nini kilichotibua makabiliano hayo.
Eneo hilo linadhibitiwa na serikali baada ya majeshi ya umoja wa Afrika kuwafurusha wapiganaji wa al Shabaab.
Maelfu ya wasomali waliotoroka makwao wangali wanaishi katika kambi za wakimbizi wa ndani kwa ndani nje ya Mogadishu.
Post a Comment