0
  
Watalii wakiondoka Sharm el Sheikh
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amewahakikishia watalii wa Uingereza na Urusi kwamba nchi yake ni sehemu salama ya kutembelea.
Katika ziara yake ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Sharm el Sheikh tangu kuanguka kwa ndege ya Urusi mwezi uliopita, Rais Al Sisi amesema Misri ni sehemu salama na imara.
Moscow imesimamisha safari zote za ndege kuelekea nchini Misri wakati uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo ya ndege ukiendelea.
Uingereza nayo imekuwa makini na safari zake za ndege katika mji huo wa Sharm el Sheikh.
Katika ajali hiyo ya ndege ya Urusi, abiria wote 224 walifariki dunia.
Baadhi ya nchi zinaamini kuwa kulikuwa na bomu ndani ya ndege hiyo.
Ikiwa ni mwezi mmoja tangu Urusi na Uingereza kusimamisha safari zake za ndege katika mji huo wa Sharm El Sheik, Misri imesema itapoteza kiasi cha dola mia mbili na nane milioni.

Post a Comment

 
Top