Meneja
Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa pili kutoka kushoto)
akishiriki katika uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO
ilitangaza kudhamini mbio za kilomita 10 kwa walemavu. Wengine kutoka
kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania Oscar Shelukindo,
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli, Mkurugenzi Msaidizi wa
Michezo katika Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni, Alex Nkenyenge
na Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha.
Meneja
Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa tatu kutoka kushoto)
akishiriki katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza uzinduzi wa
Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za
kilomita 10 kwa walemavu.
---
GAPCO, kampuni ya mafuta inayoongoza Tanzania imetangaza udhamini wake
wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016 kilomita 10 kwa walemavu.
Akitangaza udhamini huo jana wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ya
Kilimanjaro Marathon, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi
alisema GAPCO inaona fahari kudhamini mbio hizo za kilomita 10 kwa
walemavu.
“Tumeshuhudia
mbio hizi za Kilimanjaro Marathon zikikua tangu tuanze kudhamini mwaka
2011 na pia kufurahia faida wanayopata washiriki na jamii inayozunguka
maeneo ambayo mbio hizi hufanyika kila mwaka. Tunayo furaha kufanya kazi
na Wild Frontiers ambao ndio waandaaji wa mashindano haya,” alisema
Kakwezi.
“Kama sehemu ya kusaidia jamii ambayo tunafanya biashara, GAPCO Tanzania
imeamua kusaidia wanariadha ambao ni walemavu kwa kudhamini mbio ambazo
wanashiriki walemavu pekee,” alisema.
Alisema
udhamini wa GAPCO pia utahusisha usafiri, malazi na chakula kwa
washiriki kutoka Dar es Salaam na pia zawadi za pesa kwa washindi wa
mbio hizo za kilomita 10 ambazo zinafanyika pamoja na mbio nyingine za
Kilimanjaro Marathon.
Kakwezi aliendelea kusema kuwa Kilimanjaro Marathon limekua tukio kubwa
linalovutia washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania na hivyo
limesaidia sana kutangaza vivutio vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro
na pia kuwaongezea kipato wafanyabiashara wa Moshi.”.

Post a Comment