Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia)akiwa kwenye picha ya
pamoja na Zuma Mwenyekiti wa ANC ya Afrika Kusini Rais Jacob (kushoto)
na Mwenyekiti wa FRELIMO ya Msumbiji Rais Philipe Nyusi (katikati)
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na
Mwenyekiti wa Chama cha SWAPO cha Namibia Rais Hage Gengob, katika
mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza kwenye
mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa vya Kusini mwa Afrika mjini
Maputo, Msumbiji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na Makatibu Wakuu wa
vyama vya ANC, FRELIMO, MPLA, SWAPO na ZANU PF mjini Maputo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Komredi Abdulrahman Kinana katikati ya wiki iliyopita aliongoza
ujumbe wa Tanzania nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa Vyama vya Siasa
Kusini Mwa Afrika.
Mkutano huo uliohudhuriwa na baadhi
ya Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa vyama hivyo, umemalizika mwishoni mwa
wiki mjini Maputo kwa mafanikio makubwa.
Mkutano huo ulijadili masuala yaliyolenga kutatua changamoto mbalimbali za mataifa hayo na mipango ya maendeleo kwa ujumla.
Baadhi ya viongozi wa vyama hivyo
vya siasa waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa ANC ya Afrika Kusini
Rais Jacob Zuma, Mwenyekiti wa FRELIMO ya Msumbiji Rais Filipe Nyusi,
Mwenyekiti wa SWAPO ya Namibia Rais Hage Geingob pamoja na Komredi
Kinana na ujumbe wake.
Ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa
na Komredi Kinana umewajumuisha Katibu wa NEC anayeshughulikia Siasa na
Mambo ya Nje Dkt. Asha-Rose Migiro pamoja na Makatibu Wakuu wa Jumuiya
za CCM.


Post a Comment