Washirika wa
kimaendeleo wameonyesha kutoridhishwa kwao na utekelezaji wa sheria ya
uhalifu wa mitandaoni ya mwaka 2005 nchini Tanzania.
Katika
taarifa ya pamoja iliotolewa jijini Dar es Salaam,washirika hao wa
kimataifa wamesema kwamba kuna ukiukaji mkubwa wa haki muhimu katika
utekelezwaji wa sheria hiyo.Wameikumbusha serikali kuhusu ahadi yake ya kuitekeleza sheria hiyo katika hali ambayo itaheshimu haki hizo mbali na kuangazia ukiukwaji wake.
Hatahivyo visa vya utumizi m'baya wa sheria hiyo vimezua wasiwasi kutokana na ukandamizaji wa haki muhimu kulingana na taarifa hiyo ya pamoja iliotolewa na ujumbe wa muungano wa Ulaya pamoja na balozi za Ubelgiji ,Denmark,Finland,France,Ujerumani,FinlandFrance,Ujerumani,Ireland,Italy,Uholanzi Uhispania,Sweden,UingerezaCanada,Norway,Uswizi na Marekani.
Viongozi wa ujumbe huo wana wasiwasi kuhusu kukamatwa kwa wanachama wa kituo cha haki na sheria na kuchukuliwa kwa vifaa muhimu vya kiufundi.
Hatua hiyo inajiri baada ya maafisa wa polisi kuvamia na kuchukua kompyuta katika afisi inayotumiwa na shirika moja la kijamii Tanzania Civil Society Consortium on election Observation TACCEO.
Maafisa hao waliojihami walivamia afisi za shirika hilo lililopo katika maeneo ya ufukwe wa bahari wa Mbezi jijini Dar es Salaam na kuchukua kompyuta 26,laptopu mbili na simu 36 ikiwa miongoni mwa uchunguzi.
Polisi wanasema kuwa makarani hao walikamamtwa kupitia sheria ya uhalifu wa mitandaoni kifungu cha 16 kwa kuchukua na kusambaza matokeo ya urais kinyume na sheria ambayo inasema kuwa ni tume ya uchaguzi pekee yenye uwezo huo.
Lakini wanachama wa shirika hilo la TACCEO wanasema kuwa kituo hicho hakikuwa kikijumlisha kura lakini bali kilikuwa kikiweka ripoti kutoka kwa waagalizi wa uchaguzi katika majimbo tofauti.
Post a Comment