Kwenye headlines za dunia kipindi hiki huwezi kuacha kuzitaja headlines za Kiongozi wa Dini ya Kikatoliki duniani, Papa Francis kufanya ziara yake ya matembezi kwenye nchi za barani Africa… kwa sasa Papa Francis yupo Kenya
kwa ajili ya ziara yake nchini humo huku mapokezi yake yameweka
headlines kwenye vituo mbalimbali vya habari duniani ikiwemo kituo cha Fox News, Marekani.
Nimetembelea mtandao wa kijamii wa Twitter na huko nimekutana na tweets nyingi sana za mashambulizi kutoka kwa Wakenya wakilaani kauli iliyoripotiwa na kituo cha habari Marekani, Fox News kilichosema ‘Pope visists War-Torn Africa’ kauli iliyowakwaza Wakenya wengi.
Wakenya wameona waongee waweke mambo sawa kwa kukiambia kituo cha Fox News
kuwa hawana vita, wana amani na waache kuripoti taarifa zisizo sahihi…
kama kawaida ripota wako nilichukuwa time ya kuzinasa tweets za wale
wote waliochukuwa time na kuwaandikia Fox News hisia zao na kusisogeza kwako hapa chini kwenye hii post…
>>> “#SomeoneTellFoxNews
mara ya mwisho kuwa na vita, ilikuwa kwenye twitter na CNN. Mkurugenzi
wao ilibidi aombe msamaha kwa Rais wetu @UKenyatta.” <<< @WaturiWaMatu.
>>> “@SokoAnalyst
@FoxNews Fox News, ongeleeni ujinga wa Wamarekani. Hakuna vita Africa!
Siku hizi ni hatari zaidi kuishi nchi za nje! Jinga!” <<< @KavirondoGulf.
>>> “Kwanini tunagombana, #SomeoneTellFoxNews kwani hatujui kuwa @FoxNews ni habari takataka?” <<< @NaomiMutua.
>>> “#SomeoneTellFox
tunajua mnataka muwe na trend dunia nzima, lakini kipaumbele hasi kama
hiki kinamfaa Kim Kardashian na sio chombo cha habari@FoxNews” <<< @IsaacKegari.
>>> “Sijawahi
kuisikia @FoxNews leo ndio mara ya kwanza. Hiki ni kipindi cha wanyama
kinachoripoti kuhusu Mbweha, yani ni kitu kama documentary ama nini?
#SomeoneTellFoxNews“. <<< @VictorMochere.
>>> “Hawa
wajinga @FoxNews ni wepesi kuripoti takataka kuhusu Africa lakini
hawawezi kuripoti kuhusu vurugu za matumizi ya bunduki US.
#SomeoneTellFoxNews” <<< @VictorMochere.
>>> “#SomeoneTellFoxNews
nyie ni wajinga kama watazamaji wenu wanaoamini ujinga wote mnaoripoti.
Inueni miili yenu, fanyeni research na elimisheni umma wenu.” <<< @Nyarkogelo.
>>> “#SomeoneTellNewsFox hakuna sehemu nyingine ambayo tungependa kuwepo #LiveandDieinAfrika“. <<< @SautiSol.
>>> “Hizi media za nchi za nje zitajifunza lini? #SomeoneTellFoxNews“. <<< @CynthiaNyamai.
>>> “#SomeoneTellFoxNews watuombe msamaha kwa uzembe wa utoaji huu wa taarifa @foxnews“. <<< @Eric.
>>> “#SomeoneTellFoxNews Kenya sio C.A.R. Kenya ina amani kushinda Ufaransa na Chicago kwa ujumla“. <<< @Mlokole.
>>>”#SomeoneTellFoxNews kuwa #CNNWalijaribuNaWakafeli propaganda za kijinga. #KenyaIsMagical #TembeaKenya“. <<< @AhmedMohamed.
>>> “#SomeoneTellFoxNews Kenya ina amani“. <<< @Mr.Onyancha.
Post a Comment