China imetetea hatua yake ya kujenga viwanja vya ndege katika bahari ya kusini mwa China
Uchina imeishutumu
Marekani kuwa inafanya uchochezi wa kisiasa, kwa kupiga doria katika
eneo linalozozaniwa la bahari ya kusini ya Uchina.
Naibu waziri wa mashauri ya nchi za nje, Liu Zhenmin, alisema
hayo katika mkutano wa Jumuia ya nchi za Asia Mashariki, ASEAN, mjini
Kuala Lumpur, Malaysia. Marekani imetuma manowari na ndege katika eneo hilo
katika majuma ya karibuni, ikisema kuwa inataka kusisitiza uhuru wa
safari za meli
Swala kubwa katika mkutano huo ni madai ya Uchina
ya ardhi katika bahari ya kusini ya Uchina, ardhi ambayo inadaiwa na
nchi za jirani pia.
Marekani imetuma manowari na ndege katika eneo
hilo katika majuma ya karibuni, ikisema kuwa inataka kusisitiza uhuru
wa safari za meli katika bahari hiyo. Uchina imekuwa ikijenga visiwa kusisitiza madai yake.
Uchina imekuwa ikijenga visiwa kusisitiza madai yake.BBC
Post a Comment