0
 
Waziri mkuu aliochaguliwa na Rais John Pombe Magufuli leo kazi iliyobaki ni kuthibitishwa tu na wabunge

Mbunge wa jimbo la Ruangwa mh.Kassim Majaliwa Jina lake lachaguliwa kuwa waziri mkuu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado kuthibitishwa tu na wabunge kama watathibishwa ndio atakuwa waziri mkuu ......
              .......endelea kufatilia kama wabunge watamthibitisha kuwa waziri mkuu
Miongoni mwa watu wanaotajwa katika kinyang'anyiro cha kuteuliwa kuwa waziri mkuu ni mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa.
RAIS John Magufuli leo anatarajiwa kukata mzizi wa fitina wakati jina la mteule wake kwa nafasi ya Waziri Mkuu litakaposomwa bungeni na Spika wa Bunge, Job Ndugai na kisha kuthibitishwa kwa kura na wabunge.

Gumzo la nani atakuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dk Magufuli, limekuwa kubwa kabla na hata baada ya kuanza kwa vikao vya Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 11 Jumatatu wiki hii ambalo juzi lilimchagua Ndugai kuwa Spika wake.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 51 (1), inasema: “Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa na Bunge.”

Aidha, Kifungu cha (2) cha Ibara hiyo kimeweka masharti kwamba mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote vile ndani ya siku 14 baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na wabunge walio wengi kuwa Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu huyo, kwa mujibu wa kifungu hicho, hatashika madaraka yake mpaka uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za wabunge walio wengi. Kwa kuzingatia Ibara hiyo, Spika Ndugai leo asubuhi anatarajiwa kwenda katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma kupewa jina hilo ndani ya bahasha na Dk Magufuli, na jina hilo litathibitishwa kwa kupigiwa kura na wabunge, ambapo kwa mujibu wa ratiba tukio hilo litafanyika alasiri. 


                                   CV YA MH.KASSIM MAJALIWA HII HAPA

Post a Comment

 
Top