Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa
wilaya ya Liwale Ephraim Mmbaga mkoani Lindi akiongea na viongozi wa kata tatu
za Liwale mjini,Liwale B,Likongowele,Nangando wakiwemo wenyeviti wa kamati ya
ulinzi na usalama wa vitongoji,vijiji,makatibu kata,maafisa tarafa,wakuu wa
shule za msingi na sekondari,wazee maarufu,viongozi wa dini na wageni waalikwa
akiwataka wananchi wa maeneo yao kuhakikisha kuwepo kwa ulinzi na usalama kwenye kikao kilichofanyika leo kwenye shule ya msingi Kawawa.
Mmbaga alisema kila kiongozi wa kamati ya ulinzi na usalama
wahakikishie wananchi usalama wao kipindi hichi cha kampeni na siku ya uchaguzi
kupiga kura kwa usalama na haki na wapiga kura wachague viongozi wanaofaa na
wanaowataka bila kulazimishwa na amewaonya wananchi watakaosababisha vurugu
watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Aliongeza kusema kampeni ni siku 60 na kupiga kura siku mmoja
na yako maisha baada ya
uchaguzi na amewataka
wananchi kuheshimu kanuni na sheria za uchaguzi na kuwepuka vitendo vitakao
leta vurugu ili tuweza kuvuka na kupiga kura kwa usalama.
Nae mwenyekiti wa kijiji cha kuchocholokana kilichopo kata ya
Likongowele Ismaili Mbonde alitoa maoni yake kwa mwenyekiti wa ulinzi na
usalama alisema chama cha mapinduzi wameandaa kamati ya ulinzi chenye vijana
zaidi ya 80 wanafanyia mazoezi kwenye maeneo ya guest ya Mangota karibu na
ofisi ya wilaya ya chama cha wananchi CUF majira ya saa moja na nusu aliwaona
wanakimbia kukatisha maeneo ya ofisi ya cuf na wengine maghala matatu kitendo
hicho ni viashilia vya uvunjifu wa amani amemuomba mwenyekiti wa ulinzi na
usalama kikundi hicho kitavunjwa leo.
viongozi wa kata tatu za Liwale mjini,Liwale
B,Likongowele,Nangando wakiwemo wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama wa vitongoji,vijiji,makatibu
kata,maafisa tarafa,wakuu wa shule za msingi na sekondari,wazee
maarufu,viongozi wa dini na wageni waalikwa
Post a Comment