Ame
Ally 'Zungu' aliyesajiliwa na Azam FC akitokea Mtibwa Sugar, leo
ameanza rasmi mazoezi na kikosi chake hicho kipya kilichomkabidhi jezi
namba 24 iliyokuwa ikivaliwa na Gaudence Mwaikimba aliyejiunga na JKT
Ruvu.
Ame
ameungana na wenzake na kupiga matizi kujiandaa na mashindano ya kombe
la Kagame. Jezi hiyo ndiyo atakayochezea michuano mbalimbali
watakayoshiriki, lakini akatamka maneno mazito sana.
Mchezaji
huyo ambaye ni mshambuliaji, amesema ana kila sababu ya kujituma kwa
nguvu zote ili Azam ifanikiwe na hakuna kisingizio kwa sababu kila kitu
anachotakiwa awenacho mchezaji wa kisasa kipo.
“Azam
hii kweli ni profesheno, kuna kila kitu ambacho mchezaji wa kisasa
anatakiwa kuwa nacho, gym, bwawa la kuogelea, viwanja yaani mchezaji
ushindwe mwenyewe,”alisema Ame.
“Hivyo, nina kila sababu ya kufanya vizuri kuhakikisha Azam inasonga na isijutuie uamuzi
Chanzo: Tovuti ya Azam FC.

Post a Comment