0


 Na Mwaandishi wetu Nachingwea
Chama cha walimu(CWT) wilaya ya Nachingwea,mkoani Lindi kimefanya uchaguzi na kuwapata viongozi  watakaokiongoza chama hicho kwa muda wa miaka mitano huku wakimchagua tena,Bakari Ngualo kuwa mwenyekiti. 
Kwa mujibu wa Katibu wa wilaya wa chama hicho ,Aidan Mahelela  alisema kuwa katika uchaguzi huo uliofanyika hivi karibuni na kusimamiwa  na mjumbe wa kamati ya utendaji Taifa,Dionis Mbilinyi ulimchagua tena Johari Abdalah kuwa mweka hazina.
Mahelela iliwataja wengine waliochagua kuwa ni pamoja na Kerubina Mungurumo ambaye ni  mwakilishi kitengo cha wanawake wa sekondari,Hasani Mpwapwa mwakili wa walemavu na Yonas Rashidi  mwakilishi a vijana.
Wengine ni  Manufred Mmuni  mwakilishi upande wa uongozi wa idara ya elimu,Dismas Nivahe mwakilishi wa chuo cha walimu,Fatuma Ayuba  mwakilishi wa shule za awali,Hadija Ngawina na Joseph Kakinga wawakilishi wa sekondari.
Akizungumza kwenye mkutano huo wa uchaguzi Mjumbe wa kamati ya utendaji Taifa wa CWT,Dionis Mbilinyi alito mwito kwa walimu kununua hisa ya benki ya walimu ambazo zimeanza kuuzwa kwenye benki za CRDB na  kampuni ya Max malipo Africa.
“   Natoa wito kwa walimu wote mujitokeze kununua hisa ya benki yetu ya walimu kwani ndio itakuwa mkombozi wetu hasa katika kujipatia mikopo”alisema Mbilinyi.SOMA ZAIDI

Post a Comment

 
Top