Wananchi wa Kathmandu wakiwa nje ya nyumba zao baada ya tetemeko la ardhi la leo.
TETEMEKO
kubwa la ardhi katika vipimo vya richa 7.3 limeitikisa tena nchi ya
Nepal leo ikiwa ni takribani majuma mawili tangu tetemeko la awali
lililoua zaidi ya watu 8000.
Wafanyakazi huko New Delhi, India wakiwa nje ya ofisi zao baada ya kutokea tetemeko la leo.
Watafiti wanasema kuwa kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika Mji wa Namche Bazar, karibu zaidi na Mlima Everest.
Takribani watu wanne wamepoteza maisha huku wengine kadhaa wakijeruhiwa kwa mujibu wa mashirika ya kutoa misaada.
Imeelezwa kuwa tetemo hilo pia lilitikisa Mji Mkuu wa India, New Delhi pamoja na Mji Mkuu wa Bangladesh, Dhaka.
Tetemeko la awali lilikuwa katika na ukubwa wa vipimo vya richa 7.8 na lilitokea Aprili 25, mwaka huu.
Katika
Mji Mkuu wa Nepal, Kathmandu ambapo tetemeko la awali liliacha madhara
makubwa watu walionekana wakikimbia kutoka kwenye nyumba zao baada ya
tetemeko la leo.
CHANZO: BBC
Post a Comment