……………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Msumbiji
Mheshimiwa Felipe Nyusi amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mapema jana mjini Dodoma, ambapo anakuwa ni Rais wa kwanza
wa nchi hiyo kulihutubia Bunge la Tanzania.
Rais Nyusi alisema ameamua
kufanya ziara hii ya kwanza nchini na kulihutubia Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kabla ya kulihutubia Bunge lingine lolote la nchi
nyingine kutokana na uhusianao mwema ulipo baina ya nchi yake na
Tanzania. “Nina furaha sana kwa uhusiano mwema wa nchi ya Tanzania na
Msumbiji ”, alisema Rais huyo.
Akimnukuu Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius Nyerere Rais Nyusi alisema, “Msumbiji ni jirani na ni
nchi ndogo hivyo ni lazima iongeze juhudi ya kupigana hata baada ya
Uhuru, tusisahau kamwe yale tuliyopitia ili tuwe na Uhuru wa kweli ”.
Aliwataka wabunge wa Tanzania
kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kupambana na adui umaskini, na
kuongeza kuwa ameitembelea Tanzania kuona jinsi ambavyo
wanafanyakazi ya uzalendo kwa nchi yao.
Alitoa wito kwa wabunge wa
Tanzania kuchangia katika kuimarisha Uhusiano baina ya nchi hizi mbili
na kuhakikisha wanapiga vita ufisadi na ugaidi ili kuleta maendeleo na
kujenga Amani kwa ukanda huu na Afrika kwa ujumla.
Aidha, Rais Nyusi kabla ya
kuhutubia Bunge akifuatana na ujumbe wake kutoka Msumbiji alitembelea
Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma ambapo
alizungumza na mwenyeji wake Mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa
Dkt. Jakaya Kikwete na viongozi wa CCM Taifa pamoja na viongozi wa
Chama cha FRELIMO.
Rais Nyusi alisema anafurahishwa
sana na ushirikiano mzuri ulipo kati ya nchi hizi mbili tangu enzi za
kupigania Uhuru, na kuahidi kuwa mawazo mazuri yaliyotolewa na viongozi
wa mataifa haya mawili tangu uongozi wa Mwalimu Nyerere hadi Kikwete
na Samora Machel hadi Armando Guebuza yatafanyiwa kazi ili hatimaye
kusaidia kwa manufaa ya nchi hizi mbili.
Naye Rais Kikwete kwa Upande
wake, alimshukuru Rais Nyusi kwa kutembelea Tanzania mara tu baada
ya Kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo tangu achaguliwe ikiwa ni miezi 4
tu iliyopita.
“Tulikua pamoja FRELIMO
ilipoanzishwa, tulikua pamoja wakati uhuru wa Msumbiji ulivyotishiwa na
mabepari naahidi kuwa tutaendelea kuwa pamoja wakati wote, alisema
Rais Kikwete.
Rais Nyusi aliapishwa kuwa
Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Januari 16, 2015 mara baaada ya Rais
Armando Guebuza kumaliza muda wake. Rais Nyusi alianza ziara yake ya
kikazi jijini Dar es Salaam Mei 17, na baadae alitembelea Visiwa vya
Zanzibar kabla ya kuhitimisha ziara yake kwa kulihutubia Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.
Post a Comment