Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akiwa ameshika mwenge baada ya kufika mtaa wa Kisutu jijini Dar kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kuzoa taka katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na na kampuni ya Green WastePro ltd. Picha na Geofrey Adroph
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza jambo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika eneo la Kisutu jijini Dar kwa ajili ya ufunguzi wa Magari ya kisasa ya kuzoa taka.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa magari ya kufanyia usafi yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro ltd.
Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni kiongonzi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2015 , Bw. Juma Khatibu Chum (hayupo pichani).
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (kushoto) akikabidhiwa risala na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena iliyosomwa wakati wa uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala jijini Dar.
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiwa kwenye zoezi la kuweka uchafu kwenye moja ya gari la kufanyia usafi lililozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Mmoja wa viongozi wa Mbio za Mwenge akizungumza mara baada ya uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro Ltd aliwasisitiza wananchi kuendelea kutumia kampuni hiyo kwani usafi utaendelea kuimarika zaidi na zaidi.
Post a Comment