Waziri wa
Nishati na Madini,George Simbachawene akipewa maelekezo leo jijini Dar
es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba kuhusiana na
uboreshaji wa Mtambo wa umeme uliopo katika wizara ya Nishati na
Madini.
Waziri wa
Nishati na Madini,George Simbachawene akikagua Mtambo wa umeme uliopo
nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
Mitammbo ya umeme iliyopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
IFIKAPO
machi mwakani tatizo la umeme jijini Dar es Salaam itakuwa historia
kutokana na kukamilika kwa miundombinu ya mitambo ya umeme ifikapo machi
mwaka huu.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene katika
ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme ya Kurasini, Mbagala pamoja na
Kinyerezi jijini Dar es Salaam leo.
Ziara
hiyo iliyoanzia katika mitambo ya Umeme Wizarani hapo na
kuelekea,Kurasini na Mbagala ikiwa na lengo la kusogeza miundombinu ya
umeme karibu na watumiaji wa umeme.
Simbachawene
amesema kuwa kuna miradi minne ambayo mpaka sasa inafanyiwa kazi kwa
uhakika inayotegemewa kusambaza Umeme kwa watumiaji bila kuwa n
amatatizo ya umeme.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba amesema kuwa
matatizo mbalimbali ya ununuzi wa Luku za umeme nayo yanafanyiwa kazi
kwa kuyahimiza makampuni nayoshirikiana na TANESCO katika uuzaji wa
umeme ili waweze kuimarisha huduma hizo.
Post a Comment