0
Ligi kuu ya Uhispania La Liga imepigwa marufuku.
Ligi kuu ya Uhispania La Liga imepigwa marufuku.
Hatua hii inafuatia mtafaruku baina ya shirikisho la ligi kuu la Uhispania na serikali ya taifa kuhusiana na ugavi wa mapato ya haki miliki ya kupeperusha mechi.
Pande zote zimeshindwa kukubaliana kuhusu ugavi wa mapato ya matangazo ya mechi za ligi hiyo maarufu duniani.
 
Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa juma lijalo tarehe 16 mei.
Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa juma lijalo tarehe 16 mei.
Marufuku hiyo itaathiri zaidi ya wachezaji laki sita (600,000) na mechi elfu thelathini (30,000).
Kufikia hizi sasa Barcelona inaongoza jedwali la La Liga,wakiwa na alama mbili pekee zaidi ya wapinzani wao wakuu Real Madrid huku zikiwa zimesalia mechi tatu tu msimu ukamilike.
Serikali kuu imepitisha mswada mpya ambao utasimamia ugavi wa fedha zinazotokana na hati miliki ya matangazo ya mechi hizo za la Liga.
 
Marufuku hiyo itaathiri zaidi ya wachezaji laki sita (600,000) na mechi elfu thelathini (30,000)
Mswada huo unaungwa mkono na muungano wa wachezaji wa kulipwa LFP.
Mkataba uliopa sasa inaziruhusu vilabu viwili vikuu nchini humo yaani , Barcelona na Real Madrid kukubaliana kivyao kuhusu nani atapeperusha mechi zao.
Kuna madai kuwa timu hizo mbili zinatia kibindoni nusu ya mapato yanayotokana na mechi zao.
Shirikisho lenyewe limesema kuwa linafahamu hasara itakayotokea lakini halijafunga mlango wa majadiliano.

Post a Comment

 
Top