Maafisa wa serikali Mashariki mwa China wamelazimika kuzuru gereza moja nchini humo kama ilani ya kutoshiriki ufisadi.
Maafisa wa serikali Mashariki mwa China wamelazimika kuzuru gereza moja nchini humo kama ilani ya kutoshiriki ufisadi.
Maafisa
hao 70 wakiwa wameambatana na wachumba wao walilazimishwa kushinda
mchana kutwa katika gereza moja lililoko mjini Shiyan katika mkoa wa
Hubei tarehe 15 mwezi Mei.
Serikali kuu ya China ilianzisha
harakati za kukabiliana na ufisadi miongoni mwa wafanyikazi wa uma tangu
rais aliyeko madarakani Xi Jinping alipochukua mamlaka mwaka wa 2012. Maafisa hao 70 wakiwa wameambatana na wachumba wao walilazimishwa kushinda mchana kutwa gerezani
Tangu mwaka huo 2012, maelfu ya
wafanyikazi wa uma wamechunguzwa na asilimia kubwa yao kuhukumiwa jela
baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yao vibaya.
Ziara
hiyo ya lazima iligundulika baada ya shirika la kupambana na ufisadi
kuchapisha ripoti hiyo katika jarida lake la hivi punde siku ya
jumamosi.
Kulingana na ripoti hiyo ya tume ''ziara hiyo ilipaswa
kuwaonya na kuwapa fursa ya kuonja maisha ndani ya jela nyuma ya vyuma
vikubwa na madirisha yaliyoweka juu zaidi''
Picha zilizochapishwa zinaonesha maafisa hao wakuu wa umma wakiambatana na wachumba wao. Ufisadi:Maafisa walazimika kuzuru jela China
Maafisa hao walipata fursa ya
kuzungumza na maafisa wanaotumikia vifungu tofauti kwa makosa ya ufisadi
na matumizi mabaya ya madaraka yao.
Aidha walitembelea maonyesho ya picha na maandishi ya wafanyikazi wenza waliofungwa.
Tume
hiyo ya kupambana na ufisadi CCDI ilisema katika ripoti hiyo kuwa wengi
wa maafisa hao walipigwa na butwaa walipowaona maafisa waliowahi
kufanya kazi pamoja na wengine wakawachwa vinywa wazi baada ya
kuwatambua vigogo waliotamba katika enzi zao lakini sasa wakiwa ni
wafungwa. Maelfu ya viongozi wamefungwa tangu rais Xi Jinping kuanzisha kampeini dhidi ya ufisadi mwaka wa 2012
Maafisa hao walilazimishwa kusikiza sauti za maafisa waliowatangulia wakikiri makosa yao.
China
imekuwa ikiendesha kampeini kubwa ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu
wa mal ya uma huku maafisa wa uma wakitakiwa kuishi maisha yao kadri ya
mishahara yao.
Aisha wafanyikazi wa umma wametakiwa kukoma
kupokea zawadi ghali kutoka kwa wanakandarasi na watu wenye nia ya
kufanya biadhara na serikali.
Vyombo vya habari vimekuwa
vikiripoti visa ambayo maelfu ya wafanyikazi wadogo serikalini
wanakamatwa na kilele cha kampeini hiyo dhidi ya ufisadi ilikuwa
kukamatwa kwa aliyekuwa mkuu wa usalama wa ndani Zhou Yongkang.BBC
Post a Comment