0
Gari la chama cha msingi Makata Amcos aina ya Fuso likiwa limehalibiwa na vijana wanaodaiwa wa bodaboda katika kijiji cha Kigwema katika kata ya Makata wilaya ya Liwale mkoani Lindi.



 Gari la chama cha msingi Makata Amcos aina ya Fuso likiwa limehalibiwa na vijana wanaodaiwa wa bodaboda katika kijiji cha Kigwema katika kata ya Makata wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Gari la chama cha msingi Makata Amcos aina ya Fuso lenye namba T 993 BPZ likiwa limehalibiwa na kuchomwa moto na vijana wanaodaiwa madereva bodaboda katika kijiji cha Kigwema katika kata ya Makata wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Tukio hilo limetokea jana chanzo kinasemekana kuwa madereva wa pikipiki (bodaboda) na bajaji alienda kucheza mpira katika kijiji cha Mpengele waliporudi kwenye mpira kufika  katika kijiji cha Kigwema bajaji iliacha njia na kupinduka maeneo ilipopaki fuso na kudai gari hilo lilipaki karibu na barabarani walilishambulia kwa mawe na kuchoma moto lakini moto waliwahi kuuizima.

LIWALE YETU BLOG iliongea na katibu wa chama hicho cha Makata Amcos bwana Mbaraka Pange alikili kupata taarifa ya tukio hilo la kuchomwa gari hilo na jitihada zingine zigonga mwamba za kutafuta mawasiliano na vyombo vya dola baada kupiga simu kutopakikana na kukosa kujua kama kuna watu waliokamatwa kuhusiana na kutukio hilo.
Chanzo halisi kitajulikana mara baada ya kupata taarifa za kina kutoka vyombo vya dola vilivyopo wilayani Liwale.

Post a Comment

 
Top