0

 http://i.ytimg.com/vi/7SBq8-0WbN0/hqdefault.jpg

Mahsein Awadh (Dr Cheni) ambae ni muigizaji katika tasnia ya filamu nchini Tanzania,mbali na kuwa msanii wa filamu lakini pia ni mshehereshaji aja na nimekubali kuolewa.
Nimekubali kuolewa ni filamu iliyokuwa ikitangazwa kwa mda mrefu sasa bila kuingia sokoni, watu walikuwa wakisubiria kwa hamu bila kiu yao kufanyiwa utatuzi.Akiongea na mwandishi wa blog hii ndugu Lewis Mbonde, Dr Cheni alisema kwamba.
 
Nimekubali kuolewa ni filamu yangu mpya ambayo ilifungiwa na ilisitishwa kuingia sokoni kwa kuwa ilikuwa inakiuka baadhi ya maadili ya kitanzania na hapo ndipo nilipoweza kuwaelewesha wasambazaji pamoja na serikali dhamira ya yangu kutaka kuitoa filamu hii wakanielewa.Marekebisho yote yameshafanyika kila kitu kipo sawa itaingia sokoni rasmi tarehe 20/05/2015.Kwa hiyo wana jamii wote kwa ujumla wakae mkao wa kula ili waweze kuipokea filamu yangu sio ya kuikosa.
Filamu hii imebeba vitu vingi sana vyenye kuelimisha jamii na pia kuburudisha
 KIONYO CHA MOVIE

Post a Comment

 
Top