15:58 Viongozi wa jeshi wamewaamrisha maafisa wa polisi kuondoka mabarabarani.
15:55 Mwandishi Sonia Rolley, wa Radio France International anasema kuwa halaiki ya raia wamefika nje ya kituo hicho wakishangilia matukio hayo
15:50 Waandamanaji wanasemekana kuambatana na wanajeshi kuelekea katikati ya mji mkuu wa Bujumbura
15:45 Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kusikiliza hoja za viongozi wenzake.
15:40 Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Maud Julien anasema kuwa Miili ya watu watatu imeonekane katika barabara za Bujumbura
15:36 Viongozi wote wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wako Dar es Salaam kwa mwaliko wa rais Kikwete.
15:35 Rais Nkurunzinza yuko mjini Dar es Salaam Tanzania kuhudhuria mkutano wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisasa uliokuwa ukiendelea Burundi.
15:30 Maelfu ya raia wa Burundi waandamana a mabarabarani mjini Bujumbura wakishangilia tangazo hilo la ''kutomtambua'' rais Nkurunzinza.
15:20 Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
15:10 Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
15:05Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
15:00 taarifa zaibuka kutoka Burundi kuwa rais Nkurunzinza ameng'olewa'' madakani.
Ripoti kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.
Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.
Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''BBC
Post a Comment