0
Tuzo za watu 2015 zimetolewa Ijumaa hii kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa ‘surprises’ za kutosha. Mshindi mkubwa kwenye usiku huo na ambaye amekuwa surprise kwa wengi ni mtangazaji wa TBC FM, D’jaro Arungu aliyeibuka na tuzo mbili.

Millard Ayo na Salim KikekeMillard Ayo na Salim Kikeke

D’Jaro alikuwa akishindana na Millard Ayo kwenye vipengele hivyo viwili ambaye hata hivyo alishinda pia kipengele cha blog inayopendwa.

D’Jaro ArunguD’Jaro Arungu akiongea baada ya kutangazwa mshindi

“Mtu yeyote aliyekuwa anashindani halafu anaamini anaweza kupata nafasi lazima imshtue,” Millard ameiambia Bongo5.

Millard AyoMillard Ayo akipokea tuzo ya blog inayopendwa

“Lakini inakushtua kwa njia nzuri kwamba kuna kitu kimemiss au labda unatakiwa ufanyie kazi zaidi. Lakini pia kura zinamata, inachangia sehemu zote, inawezakana ubora wa kipindi na kura pia. Lakini all in all mimi nampongeza sana D’Jaro Arungu, ameshinda kura zote mbili, ni changamoto pia, inatupa nafasi sisi wenyewe kushindana lakini inasaidia pia kufanya kazi kwenye biashara yetu vizuri.”

Wema Sepetu aliyekuwa ametajwa kuwaniwa vipengele vitatu ameibuka na tuzo moja.

Wema Sepetu Wema Sepetu akipokea tuzo yake ya muigizaji wa filamu anayependwa

“I’m Grateful… I’m humbled…. I’m out of words… Ila nawapenda for making this happen…. Shout out to all my fans out there… Na haters pia…. I say it’s a new beginning.”

“Therez more to this…. I take it as a challenge and a wake up call to give you guys more of what you want me to give,” ameandika Wema kwenye Instagram baada ya ushindi huo,” aliongeza Wema.

Ray Ray akishukuru baada ya kutangazwa mshindi wa kipengele cha muongozaji wa filamu anayependwa
Dada wa Alikiba
Dada wa Alikiba akipokea tuzo kwa niaba ya kaka yake
Lady Jaydee
Lady Jaydee akishukuru baada ya kushinda tuzo ya mwanamuziki wa kike anayependwa
Ommy DimpozMiss Tanzania 2014/15, Lilian Kamanzima akimkabidhi tuzo Ommy Dimpoz
tuzo za watu 2015
Shangwe kwa washindi
Jacqueline Mengi na Nasreen KarimJacqueline Mengi na Nasreen Karim ni miongoni mwa waliohudhuria
Luca na Nancy
Luca na Nancy wakizungumzia tuzo za watu 2015

Hii ni orodha kamili ya washindi

Mtangazaji wa redio anayependwa

D’Jaro Arungu – TBC FM
Kipindi cha redio kinachopendwa

Papaso – TBC FM
Mtangazaji wa runinga anayependwa

Salim Kikeke – BBC Swahili
Kipindi cha runinga kinachopendwa

Mkasi – EATV
Blog/Website inayopendwa
Millardayo.com
Muongozaji wa video anayependwa
Hanscana
Muongozaji wa filamu anayependwa
Vincent ‘Ray’ Kigosi
Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa
Wema Sepetu
Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa
Hemedy PHD
Mwanamuziki wa kike anayependwa
Lady Jaydee
Mwanamuziki wa kiume anayependwa
Alikiba
Filamu inayopendwa
Kigodoro
Video ya muziki inayopendwa

Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz

>>BONGO5

Post a Comment

 
Top