Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Fortunata Raymond akitoa
elimu kuhusu maboresho yanayoendelea kufanywa na mfuko mbele ya viongozi
na wawakilishi wa chama cha walimu mkoa wa Lindi,wakati wa mkutano wa
mwaka wa chama hicho,ambapo alisema kwa sasa katika kukabiliana na
changamoto ya huduma ya dawa mfuko umeanzisha mkopo wa dawa na
vitendanishi kwa vituo vilivyosajiliwa na mfuko, ambapo bodi ya
wakurugenzi iliridhia kutolewa kwa mikopo hiyo tangu mwezi Oktoba.2014.
Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Chamikumbi mkoani hapa.
Wajumbe wa mkutano wa mkuu wa chama cha waalimu mkoa wa Lindi
wakimsikiliza meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya (hayupo pichani)
Fortunata Raymond wakati akifafanua mikakati mbalimbali inayotekelezwa
na mfuko katika kuhakikisha wanachama wa mfuko wanapata huduma stahiki
na bora zaidi.
Fabiani Erioh mwakilishi wa shule za msingi Lindi vijijini kwenye
mkutano mkuu wa viongozi wa CWT, akitoa hoja baada ya mada
zilizowasilishwa kutoka kwa mwezeshaji wa mfuko wa Taifa wa Bima ya
afya.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Lindi Ramadhan Mtumwa
akifafanua mafao yanayotolewa na mfuko huo mbele ya viongozi wa CWT
mkoani hapa,ambapo alibainisha ubora mafao hayo kama vile fao Elimu,fao
la uzazi,mikopo ya nyumba sanjari na mkopo wa kuanza maisha pale
mwanachama wa mfuko anapopata ajira,hivyo alitoa wito kwa wanachama
kuiona kuwa ni fursa.
Kutoka kulia ni meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya Fortunata
Raymond akichukua dondoo za hoja kutoka kwa wanachama wa mfuko,kushoto
ni meneja wa PSPF Ramadhan Mtumwa mkoani Lindi akifuatilia kwa karibu.
Post a Comment