Cristiano Ronaldo akiruka juu kupiga kichwa mpira
LIGI ya mabingwa barani ulaya imeendelea usiku huu kwa mechi mbili za robo fainali kupigwa.
Uwanja wa Vicent Calderon, Atletico Madrid wametoka suluhu (0-0) dhidi ya mahasimu wao wa jiji, Real Madrid.
Matokeo haya yanawaweka Atletico Madrid kwani watahitaji kufanya kazi ya ziada katika dimba la Santiago Bernabeu.Real
Madrid walicheza vizuri na kutengeneza nafasi kadhaa ugenini, lakini
wenyeji walikuwa butu safu ya ushambuliaji kitu kilichowafanya wakose
ushindi.
Katika dakika 90′ Real Madrid wamepiga mashuti 8 yaliyolenga lango dhidi ya mawili ya Atletico.
Mbali na hivyo vijana wa Carlo Ancelotti walimiliki mpira kwa asilimia 52 dhidi ya 48 za wenyeji.
Kutokana na presha waliyotoa Real, Atletico wamelazimika kufanya madhambi mara 19 dhidi ya 11 ya vijana wa Bernabeu.
Jumatano
ijayo, Real Madrid wanahitaji ushindi wa goli 1-0 au 2-1 ili kusonga
mbele na kama Atlectico wanahitaji kusonga mbele nao wanahitaji ushindi
kama huo au ushindi.
Wakitoka 1-1, Atletico atasonga mbele kwa faida ya goli la ugenini.
Mechi nyingine usiku huu, Juventus wameshinda goli 1-0 dhidi ya Monaco.
Goli la Monaco limefungwa na Arturo Vidal kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 57.
Juventus wanahitaji suluhu (0-0) ugenini ili kusonga mbele.
UEFA
itaendelea tena leo kwa robo fainali mbili kupigwa, FC Porto
wanaikaribisha Bayern Munich, wakati Paris Saint Germain wanaikaribisha
FC Barcelona.
Post a Comment