Nembo ya Tume ya Uchaguzi Tanzania, chini yake ni mwanamke mmoja akimsaidia mwenzake kumwonyesha sehemu ya kupiga kura
Tume
ya uchaguzi nchini Tanzania imesogeza mbele kwa wiki moja zaidi tarehe
ya kuzinduliwa kwa zoezi la daftari la wapiga kura litakalotumia mfumo
mpya wa kieletroniki yaani Biometric Voters Registration BVR. Zoezi hilo
ambalo litaanza rasmi katika mkoa wa Njombe na baadae kufuatia katika
mikoa mengine ya Tanzania hivi sasa linatarajiwa kuanza tarehe 23 ya
mwezi huu badala ya tarehe 16 kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi nchini humo amesema lengo la mabadiliko hayo ni
kuvipa fursa vyama vya kisiasa kujiandaa na kuandaa watu wake. Hata
hivyo, baadhi ya viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa wamesema kauli hiyo
haina ukweli wowote na kwamba tume inajikosha kwa sababu haina vifaa
vya kutosha vya kuendesha uandikishaji huo.KUSOMA ZAIDI HABARI HII BOFYA HAPA
Post a Comment