Mashirika
mbali mbali ya kiraia nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameomba
majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini humo MUNUSCO
kufikiria upya mpango wake kujiondoa kupambana na kundi la waasi la
FDLR.
Hapo jana majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa
yaliyopo Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo yalitangaza kujiondoa katika
operesheni hiyo kwa kushirikiana na majeshi ya serikali ya DRC hadi hapo
serekali ya Kongo itakapotengua uteuzi wa majenerali wawili
walioteuliwa kuongoza opereshini hiyo.Kwa mujibu wa MUNUSCO majenerali hao wana tuhumiwa kufanya vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Post a Comment