0
                    Mkutano wa mkuu wa mkoa wa Lindi na waendesha bodaboda wilayani Liwale
                           Ziara ya mkuu wa mkoa wa Lindi mh.Mwantum Mahiza wilaya Liwale
LIWALE-LINDI
Mkuu wa Mkoa wa Lindi bi.Mwantum Mahiza amefanya ziara wilayani Liwale ameweza kuongea na waendesha pikipiki (bodaboda) wakisoma lisara yao waendesha pikipiki kwa mkuu wa mkoa walitoa changamoto zao ambazo wanakumbana nazo katika shughuli zao za kila siku.

Changamoto wanazokumbana nazo kama kukosa mitaji ya kuendeleza shughuli zao,kukosa ofisi ya waendesha pikipiki kwani ofisi inatumika sasa ni ya kupanga hivyo kwakuwa mtaji wao mdogo watashindwa kulipia pango pia changamoto nyingine kuhusiana na usalama wao kuwa mdogo nyakati za usiku wakati wanapowapeleka wateja ambao wanawatilia mashaka.

Mkuu wa mkoa akijibu lisara hiyo aliwahaidi kuwapatia uwanjwa ambao watajenga ofisi yao,suala la kukosekana kwa mtaji aliwahadi atawakopesha pikipiki kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii  na suala la usalama alisema endapo mtu watamtilia mashaka watoe taarifa haraka kwenye vyombo vya dola.

Licha ya hayo mkuu wa mkoa aliwaomba vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na kushiriki kuipigia kura rasimu ya katiba iliyopendekezwa kwa kuikubali.


Post a Comment

 
Top