Mwaandishi wetu
Wananchi
wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi wametakiwa
kutii na
kutekeleza matakwa ya sheria ili kuhakikisha haki ya kila mtu
inatendeka
na kuweza kuishi bila kubughudhiwa na mtu.
Hayo yameelezwa leo Kilwa masoko na hakimu mkazi
mfawidhi wa
mahakama ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,Arcard
Chuwa,kwenye
sherehe ya maadhimisho ya siku ya sheria duniani.
Chuwa alisema kila mtu anawajibu wa kutii na kutekeleza matakwa
ya sheria zilizowekwa ili kila raia aishi katika njia ambazo hazita
wabugudhi na kuwadhulumu raia wengine.
Alisema mahakama hazina haki ya kukataa sheria zilizotungwa na
bunge kwani chombo hicho kinawakilisha wananchi,hivyo kama
sheria imetungwa ni dhahiri wananchi wenyewe wameitaka na
kuiridhia sheria hiyo.
Chuwa alisema ilihaki iwepo ni lazima kuwepo na sheria nzuri
na za haki,hivyo ni wajibu wa mahakama,serikali na wadau
wengine kuhakikisha sheria inafuata misingi ya haki." haki ni
jambo muhimu katika kuchunguza chanzo cha sheria na
kusimamia
:
wake,kama haki haipo itakuwa ni sheria yenye nguvu tu
wake,kama haki haipo itakuwa ni sheria yenye nguvu tu
"ndiyo maana marehemu Shaaban Robert alisema waweza
kuichovywa hatia yako katika dhahabu upendavyo lakini
mkuki imara wa haki hauvunjiki,"alisema Chuwa.
Kwa upande wake
mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya
Kilwa Ali
Mtopaalisema walisema udhaifu katika kutoa
hukumu
unasababisha raia kujichukulia sheria mkoni.
Ali Mtopa alisema hukumu zisipotolewa kwa haki zinakuwa
ni chanzo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi baada
ya kuona maamuzi yaliyotolewa yanawafanya wahalifu kuwa
huru na kuendelea kutenda uhalifu.
Post a Comment