Viongozi
wa mataifa ya Ulaya wamesema kuwa wataiwekea vikwazo zaidi Urusi iwapo
itashindwa kusimamia makubaliano mapya yaliyofikiwa kusitisha mapigano
Mashariki mwa Ukraine.
Kansela wa Ujeruman Angela Merkel amesema
kuwa tayari mataifa hayo yalishakubaliana vikwazo hivyo itakavyo wekewa
Urusi iwapo itakiuka makubaliano hayo. Markel aliyasema hayo muda mfupi
baada ya viongozi hao wa Ulaya kuwasilisha makubaliano yanayo zihusisha
Ukaraine na Urusi kufuatia machafuko yanayoendelea. Usitishaji wa
mapigano mashariki mwa Ukraine unatarajiwa kuanza rasmi Jumamosi
usiku,hata hivyo wanajeshi wa Ukraine na Waasi wa Urusi wapo katika hali
ya wasiwasi kufuatia makubaliano hayo mapya huku kila upande ukiangalia
mwingine katika utekelezaji wa kuelekea kuleta Amani mashariki mwa
Ukraine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment