Matumizi
ya mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram ni kitu
ambacho kimeshika chati sana kwa sasa duniani, vijana wameonekana kuwa
waathirika wakubwa wa matumizi ya mitandao hii.
Kijana Little Wang ambaye
umri wake ni miaka 19 huko China aliona njia pekee ya kukomesha tabia
yake ya kupenda kutumia laptop na simu kuingia mtandaoni ni kujikata
mkono wake, alipoona hali haimwendei sawa aliita taxi impeleke Hospitali
ambapo hakuna aliyejua kinachoendelea nyumbani kwao, aliacha ujumbe
kwamba ametoka kwenda Hospitali na angerudi muda mfupi baadaye.
Madaktari walimfanyia operation kuunga
mkono huo huku wakiwa na matumaini kwamba baadae utaweza kufanya kazi
kama ilivyokuwa mara ya kwanza kabla hajaukata.
Mama yake Little alisononeshwa na kitendo hiki na kusema hakutegemea mtoto wake angeweza kujifanyia ukatili wa aina hii.
Post a Comment