0
Ni tukio lisilo la kawaida na la kusikitisha sana lililotokea katika kijiji cha Songambele wilayani Mlele mkoani Katavi watu wasiofamika wamemvamia  na kumuuwa mwenyekiti wa kijiji hicho cha Songambele na kisha kutenganisha kichwa na kiwiliwili na pia sehemu zake za siri na kukatwa mkono wake mara mbili.Baada ya kutenda unyama huo walichukua viungo walivyokata na kisha kuvitia kwenye sufuria  wakaweka maji na kisha kubandika kwenye moto na kuanza kuvipika.
 Baada ya kufanya tukio hilo watu hao walitokomea sehemu isiyofahamika na Polisi wilayani mlele wanaendelea na uchunguzi ili kubaini wahusika wa tukio hilo.Tukio hilo limetokea usiku wa leo majira ya saa saba usiku.

TUNAOMBA RADHI PICHA HATUTAZIWEKA KWAKUWA ZINATISHA.

Post a Comment

 
Top