wakulima na wafugaji yaliyotokea wiki
iliyopita katika Kata za Matui na Kiperesa wilayani hapa. Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Manyara, Deusdedit Nsimeki amesema bado wanaendelea na
uchunguzi kabla ya kuchukua hatua ya kuwafikisha mahakamani watu hao.
“Hatuwezi kutaja idadi kamili wala majina yao ila ni zaidi ya watu 13
tunawashikilia, wanadaiwa kuhusika na tukio hilo la mauaji na baada ya
uchunguzi wetu wahusika tutakaowabaini tutawafikisha mahakamani,”
alisema.
Hata
hivyo, jana na juzi hali ilikuwa shwari katika eneo hilo huku wakazi
wilayani humo wakishuhudia helikopta ya polisi ikiwa na makamishna
kutoka Makao Makuu ya Polisi, Dar es Salaam ikizunguka angani kuendelea
na ulinzi.
Naye,
Mkuu wa Mkoa huo, Eraston Mbwilo akizungumza kwenye kikao cha ushauri
cha mkoa, alisema chanzo cha mgogoro wa ardhi na mauaji hayo ya Kiteto
yanasababishwa na baadhi ya watu kuhodhi ekari za ardhi bila ya kuwa na
vibali. “Hili suala la baadhi ya watu kudai kuwa Kiteto imegeuka kuwa
Somalia siyo kweli, mgogoro wa Emboley Murtangos unasababishwa na baadhi
ya watu kujimilikisha ekari nyingi za ardhi kiholela,” alisema Mbwilo
na kuongeza: “Unamkuta mtu anamiliki ekari zaidi ya 500 kiholela, huu ni
ukiukwaji wa sheria, vijiji vina utaratibu wa kugawa maeneo, kwa nini
wasiufuate?” alihoji. Alisema kwa sasa hali ni shwari katika eneo hilo
na wanaendelea kufanya mazungumzo na viongozi wa jamii ya wakulima na
wafugaji ili kuhakikisha kuwa mauaji na vurugu hizo havitokei tena.
Post a Comment