mwaandishi wetu Liwale….
Baadhi ya Wananchi wa
Liwale mkoani Lindi wamesema wamekataa tamaa na hali ya maisha ya
yao kutokana na kukosa huduma muhimu zap kijamii ikiwemo maji safi,
mawasilino na huduma bora za afya
Akizungumza kwa niaba ya
wananchi wa kijiji cha Ngunja na Lilombe wilaya humo Mwajuma Mkombe
alisema kuwa maisha ya wananchi yamekuwa ya kubahatisha kama
wanyama kila kukicha hali inakuwa ngumu afadhali ya jana kwani, kilimo
kama nguzo kuu ya kiuchumi kwao, kimekuwa hakiwaletei tija yoyote.
“Ni hatari ukifika
vijiji vya Ngunja, Lilombe, Ngogowele ukawauliza wakulima wanachohitaji
utawasikia wakilalamika shida yao ni ukosefu wa soko la uhakika la
mazao na uhaba wa pembejeo. Mawasiliano na huduma za kijamii, afya na
maji.
“Hawajui nani atawajibika
kuwalipa japo fidia kidogo ya hasara waliyopata. Baada ya kukosa soko
la uhakika mazao yao ikiwemo korosho mahindi na upunga,upande wa elimu,
ni shida shule chache, walimu hawatoshi, maabara hakuna huku umbali
ukiwa kikwazo kwa wanafunzi wa baadhi ya maeneo," alisema
Post a Comment