Shirika la Hisani la Madaktari Wasio na Mipaka – MSF limesema litazindua
majaribio ya kliniki ya aina tatu ya dawa za kutibu ugonjwa wa Ebola
katika eneo la Afrika Magharibi kuanzia mwezi ujao wa Desemba. Majaribo
hayo yatafanyika nchini Liberia na Guinea. Ni habari za kuwapa matumaini
wagonjwa katika juhudi za kutafuta dawa kamili ya Ebola, ugonjwa hatari
unaoua kati ya asilimia 50 na 80 ya watu walioambukizwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

Post a Comment