MAOFISA
wawili wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) waliokuwa wakisafirisha fedha
kutoka Mwanza kuelekea Shinyanga, wamefariki dunia baada ya ajali ya
gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali.Chanzo
cha ajali hiyo kimeelezwa ni baada ya gari hilo lililokuwa likiongoza
msafara wa magari ya BOT kupinduka baada ya kumgonga mwendasha pikipiki.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, alisema ajali hiyo
ilitokea jana saa 7:45 mchana katika barabara ya Mwanza - Shinyanga,
eneo la Bohari, kata ya Butimba.
Kamanda Mlowola aliitaja pikipiki iliyosababisha ajali hiyo ni yenye namba za usajili T 792 CTG. "Baada
ya pikipiki kuingilia msafara huo, iligongwa na gari la ulinzi
lililokuwa kwenye msafara huo aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za
usajili SU 3526 mali ya Benki Kuu"
Kabla
ya ajali hiyo, dereva wa gari la ulinzi alijaribu kumkwepa mwendesha
bodaboda, lakini kutokana na msafara huo kuwa na mwendo mkali,
lilipasuka tairi la mbele na kukosa mwelekeo hivyo kupinduka.
"Pamoja
na ajali hiyo, magari yaliyokuwa yamebeba fedha yapo salama, hakuna
upotevu wowote wa fedha kwasababu askari waliokuwa kwenye magari mengine
walichangamka na kuimarisha ulinzi wakishirikiana na askari wa JWTZ"
alisema Kamanda Mlowola.
Kamanda
aliwataja waliofariki katika ajali hiyo ni dereva wa gari lililopata
ajali Mohamed Mumba na Beatrice Lumelezi ambaye ni Ofisa wa BOT.
"
Majeruhi ni watatu ambao kati yao ni askari wawili pamoja na dereva wa
bodaboda ambaye nimeelezwa kuwa ana hali mbaya. "Miili ya waliofariki
imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando na majeruhi wamelazwa
hospitalini hapo kwa matibabi zaidi" alisema. SOURCE:G SENGO
Post a Comment