MANCHESTER
United imeendeleza ubabe dhidi ya Arenal, baada ya usiku huu kuichapa
mabao 2-1 Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2837001/Arsenal-vs-Manchester-United-Team-news-kick-time-probable-line-ups-odds-stats-Premier-League-clash.html#ixzz3JpEIaEU5
United
walipata bao la kwanza dakika ya 56, baada ya beki Kieran Gibbs
kumfunga mwenyewe kipa wake, Wojciech Szczesny katika harakati za kuokoa
krosi ya Antonio Valencia, kabla ya Nahodha Wayne Rooney kufunga la
pili dakika ya 85 akimalizia pasi ya Angel di Maria. Olivier Giroud
aliifungia Arsenal la kufutia machozi dakika ya 90.
Beki
wa United, Luke Shaw alitolewa nje dakika ya 16 baada ya kuumia kifundo
cha mguu, wakati kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere alinusurika kupewa
kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Marouane Fellaini.
Lakini
kiungo huyo wa England alitolewa nje dakika ya 55 baada ya kuumia pia.
Kipa Szczesny pia alitolewa uwanjani baada ya kuumia.
Kikosi
cha Arsenal kilikuwa; Szczesny/Martinez dk59, Chambers, Mertesacker,
Monreal, Gibbs, Ramsey/Giroud dk77, Arteta, Wilshere/Cazorla dk55,
Oxlade-Chamberlain, Welbeck na Sanchez
Manchester
United; De Gea, Smalling, McNair, Blackett, Valencia, Carrick,
Fellaini, Di Maria, Shaw/Young dk16/Fletcher dk89, Rooney na Van
Persie/James Wilson dk75.
Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney (kulia) akishangilia baada ya Kieran Gibbs kujifunga
Woljciech Szczesny na Kieran Gibbs wa Arsenal wakipamiana kabla ya kujifunga
Post a Comment