| Mkurugenzi
wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki akizungumza na
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youqing alipofika Wizarani
tarehe 10 Novemba, 2014 kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao Mhe. Lu
aliishukuru na kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa msimamo wake kuhusu
tuhuma dhidi yake na China kuhusu biashara haramu ya pembe za ndovu na
pia alisifu jitihada za Serikali ya Tanzania katika kupambana na
biashara hiyo na kusema China inaunga mkono jitihada hizo na ipo bega
kwa bega kuhakikisha inatokomezwa kabisa. |
Post a Comment