0

Waumini wa dini ya kikristo dhehebu la wasabato wakiwa wameshikilia biblia mara baada ya kubatizwa wakati wa mkutano wa injili wa wanavyuo vikuu na kati vya Union ya kusini mwa Tanzani (TUCASA) wenye lengo la kujifunza maandiko matakatifu ya biblia ulioenda sambamba wa upimaji wa afya kwa watu 311 kuchungwa magonjwa mbalimbali uliofanyika kwa siku 20 katika uwanja wa shule ya msingi Mwembesongo Manispaa ya Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG
Viongozi wa mkutano huo na wenyewe wakiimba.

Mwalimu wa chuo cha Jumuiya ya Waislamu Ahamadiyya mkoa wa Morogoro, Ustadh Shamuna Juma akitoa mawaidha wakati wa mkutano wa injili wa wanavyuo vikuu na kati vya Union ya kusini mwa Tanzani (TUCASA) wenye lengo la kujifunza maandiko matakatifu ya biblia ulioenda sambamba wa upimaji wa afya kwa watu 311 kwa kuchunguzwa magonjwa mbalimbali uliofanyika kwa siku 20 katika uwanja wa shule ya msingi Mwembesongo Manispaa ya Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG

Baadhi ya waumini wakifuatilia matukio katika mkutano huo.


Juma Mtanda, Mwananchi.
Morogoro.
Zaidi ya watu 300 mjini hapa, wamechunguzwa afya, ili kuwawezesha kujua nafasi zao katika magonjwa mbalimbali.


Watu hao walifanya hivyo wakati wa Mkutano wa siku 20 wa Injili, ulioandaliwa na Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na vya Kati wa Madhehebu ya Wasabato Kusini mwa Tanzani (Tucasa).
Mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Mwembesongo, mjini Morogoro, ulilenga kuwawezesha washiriki kujifunza maandiko matakatifu ya Biblia.


Mmoja wa madaktari walioshiriki katika uchunguzi, Dk Nyanswi Mwita alisema wananchi hao walichunguzwa malaria, maambukizi katika njia ya haja ndogo, wingi wa damu, Ukimwi, kisukari na shinikizo la damu.


Alisema watu waliobainika kuwa na maradhi, walipewa tiba na ushauri kuhusu namna ya kukabiliana na magonjwa yanayowasumbua.


Dk Mwita alisema pia walitoa dawa za kinga za matende, mabusha na minyoo.


Alisema kimsingi mkutano huo uliomalizika juzi, ulikuwa na malengo mengi ikiwa ni pamoja na kuwajenga wanafunzi kiroho.


Alisema ingawa walijikita zaidi katika mafundisho ya dini ya Kikristo, lakini pia kulikuwa na vipindi vya mahusiano ya dini, kati ya Waislamu na Wakristo.


Washiriki walitoka katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa na Dodoma.

Post a Comment

 
Top